ongea kwa sauti

Youth4Nature Kampeni ya Hadithi: Maelekezo ya Uwasilishaji 

Kusudi:

Tunaamini ya kwamba vijana wana hadithi zenye nguvu na za kulazimisha ili kushiriki kuhusu uhusiano baina ya asili na mgogoro wa tabia ya nchi. Hivyo, Youth4Nature yawaita vijana wote kutoka ulimwenguni kote watume hadithi zao kuhusu ufumbuzi wa asili. Tunajenga jukwaa kwa ajili ya sauti za vijana ili kusikika na mitazamo yao kushirikishwa. Lengo letu ni kuinua sauti za vijana, kuziimarisha katika mitandao, na kujenga uwezo wao ili wawe mawakili wa harakati za “asili kwa tabia ya nchi”. Hadithi zitashirikishwa kwenye mtandao katika vyombo vya habari mbalimbali, na pia kupitia vyombo vya kidigitali na kijamii.

Tunatazamia pia kuchagua wanahidithi kadhaa ili kushirikisha hadithi zao katika ukumbi wa kimataifa kupitia kuungana na wawakilishi wa Youth4Nature kwa Mkutano wa Katibu Mkuu wa Muungano wa mataifa kule New York mwezi wa Septemba!

Ni nini tunachokitafuta( na tusichokitafuta):

Tunawatafuta vijana ili washirikishe uzoefu wao katika ardhi na maji wanaoishi katika, na vile ardhi na maji hayo yameathiri juhudi zao kwa hatua za tabia ya nchi. Haswa, tunatafuta hadithi za vijana wanaoshiriki na ubunifu wa asili katika mashinani na katika jamii zao.

Tunatafuta hadithi za kibinafsi, zinazoshawishi na zinazo sauti zenye nguvu, ambazo zinaambatana na jamii na maeneo. Hadithi zapaswa kuwa na mtazamo wa makao ya ndani, na anayehadithia anapaswa kuonyesha uhusiano kwa kwanza na ardhi na maji ya ndani. Hadithi pia ziwe zinaeleweka kwa uhusiano na asili pamoja na mgogoro wa tabia ya nchi, haswa kupitia mtazamo wa suluhu.

Tunahimiza mchanganyiko wa hadithi kuhusu ubunifu wa asili! Hadithi kuhusu misitu, maji na mazingira ya pwani,kilimo na chakula, jangwa na udongo, asili ya mijini, na maarifa ya mitaa na ya kienyeji yamekaribishwa.

Baadhi ya maswali ya kuelekeza ili kukusaidia kuwasilisha hadithi ni kama:

 • Asili imechangia jinsi unavyo fikiri kuhusu na kukabiliana na mgogoro wa tabia ya nchi?

 • Ni ubunifu upi wa asili una uwezo wa kurejesha mazingira na kudhibiti tabia ya nchi katika jamii yako?

 • Umehusika katika kueneza ubunifu was asili katika jamii yako? Ulipata funzo/mapitio gani? Changamoto zilikuwa zipi? Kilichokusaidia sana katika utelekezani ni nini?

 • Kutokana na mapitio yako binafsi, ni vipi wanasheria wa kitaifa na ndani wanaweza kusaidia ufumbuzi wa kiasili?

Hatutafuti:

 • Insha au vipande vya kinadharia kuhusu mgogoro wa tabia ya nchi na ubunifu/ suluhu za asili;

 • Magazeti ya kitaaluma;

 • Hadithi za watu wengine, au kuhusu mchango/ mipango ambayo anayehadithia hakuhusika, au kuwa na uhusiano wa moja kwa moja;

 • Taarifa au maoni kuhusu jinsi sisi, kama jumuishi la dunia, tunapaswa kufanya;

 • Hadithi kuhusu ufumbuzi wa mgogoro wa tabia ya nchi ambazo haziambatani na asili ( mfano, technologia ya Kawi safi, usafiri endelevu, mikakati ya uchumi wa mviringo, na kadhakila.)

Tunahimiza hadithi za kweli na za kibinafsi ambazi zitashirikisha ulimwengu jinsi vijana wana thamani ya asili licha ya mgogoro was tabia ya nchi na vile vijana wanaongoza katika kutimiza ufumbuzi wa asili katika kiwango cha ndani. Kama asili imehamasisha vitendo vyako katika mgogoro wa sasa wa tabia ya nchi, tunataka kuvisikia( na vijana wengi katika dunia)! Mengi yameshirikishwa kuhusu mgogoro wa kimataifa wa tabia ya nchi na kuhusu mambo ambayo tunapaswa kuwa tukiyafanya. Sasa twakutaka ushirikishe hadithi yako ya binafsi na ya ndani. Fanya matendo yako yatoe tumaini na kuhamasisha ufumbuzi katika na kwa vijana dunia mzima.

Fomu ya uwasilishaji

Miongozo ya jumla

 • Wanaoshiriki lazima wawe vijana wa miaka 18-30 ( waliozaliwa katkati ya miaka 1989 na 2001)

 • Uwasilishaji wawezwa kufanywa na mtu binafsi au makundi. Iwapo uwasilishaji ni wa makundi, mtu mmoja tu ndiye atakaye pendekezwa kwa mkutano wa UNSG. Ni jukumu la kila kikundi kuamua mwakilishi wao.washirika wote lazima wawe vijana.

 • Wasilisho moja tu linakubalika kwa kila mshirika. Iwapo wasilisho lilikuwa la kikundi, hilo litahesabika kama wasilisho moja

 • Tunakubali mawasiliano ya kuona na ya maandishi, pajona na picha, video na machapisho ya blogu;

 • Hadithi lazima ziwekwe moja kwa moja kama faili. Namna za faili zinazokubalika ni kama:

Video: MP4 (.mp4), Windows Media Video (.wmv), Flash Video (.flv), AVI (.avi), and        QuickTime (.mov).

                            Picha: JPEG (.jpg and .jpeg), PDF (.pdf) and PNG (.png).

             Maandishi: Microsoft Word file (.doc and .docx), and PDF (.pdf).

 • Faili zote zinazowekwa lazima zipewe lebo sahihi, na ziwe na jina la anayewasilisha. Tafadhali fuata huu mtindo: “Jina_Maelezo.faili”

                                  Mfano. “MarinaM_Kulinda-Misitu-Canada.mp4”

 • Mawasiliano yapaswa kuambatana na viwango vifuatavyo:

                 Uwasilishaji wa video:

 • Iwe na urefu wa dakika tano(5)

 • Irekodiwe kwa muundo wa mazingira

 • Hadithia- video zinazohusisha mtu mmoja au zaidi akiongea katika sehemu moja muda wote hazipendekezwi( tumia mtandao vyema!);

 • Iwapo sehemu, au kwa ujumla, maeneo ya uzungumzaji yako katika lugha ambayo si kiingereza, weka pamoja vichwa ya kiigereza. Tunawahimiza wawasilishaji kuchukua video za hadithi kwa lugha ya mama /lugha ambayo matendo yanafanyika, ila tafadhali ongeza vichwa vya kiingereza.

 • Uwasilishaji wa picha: hakikisha kuna taarifa inayoambatana na picha, kwa maneno yasiyozidi 200 , kwa kila picha unayowasilisha. Faili za picha lazima zipewe uandikishaji wa kutosha na kuambatanishwa na maandishi/ taarifa kamili;

 • Kwa hadithi za kuona, hakikisha umeambatanisha na taarifa/maandishi yanayoeleza muktadha wake

 • Uwasilishaji wa maandishi:

 • Hadi maneno 1500

 • Fuata mkondo wa kuhadithia: Iwe na mwanzo, mwili na hatima, na peana hadithi ya kibinafsi kwa sauti ya kuvutia;

 • Hakikisha kichwa cha hadithi kimeeleweka kwa urahisi;

 • Unapo nukuu matamshi ya wengine hakikisha inaonyesha vyema

 • Mawasilisho yote yawe ni kazi halisi ya m(wa)tunzi.unapowasilisha hadithi iliyochapishwa hapo awali, lazima hadithi yenyewe iwe imesasishwa kwa namna fulani, kiungo cha uchapisho cha awali kuambatanisha katika uwasilishaji.

 • Hadithi sote zichapishwe kwa kiingereza. Hata hivyo, tunahimiza uwasilishaji katika lugha zingine, ikiwepo Kifaransa, Kirusi, Kihispania, Kireno, Kiitaliano, Kiholanzi,Kiswahili, Kihindi na Kiurdu. Iwapo utawasilisha katika lugha hizi, hadithi yako itachapishwa nasi mara mbili: wasilisho halisi kwa lugha halisi na nyingine katika kiingereza. Iwapo katika lugha ambayo sio kiingereza, tunawahimiza pia kupeana tafsiri  ya kiingereza( katika maandishi, rekodi ya sauti, vichwa) ili kukinga kupotoshwa katika tafsiri.

 • Tunahimiza vichwa vya kiingereza katika uwasilishaji wa video, pindi lugha zingine zonapotumika.

 • Lugha zingine pia zitaweza kukubaliwa, ila wasiliana na Youth4Nature ili kuelezwa zaidi.

Ndani ya mipaka hii, unaweza kuwa mbunifu jinsi upendavyo. Fikiria wasikilizaji wako: vijana ambao wanatarajia kupewa motisha na wenzao.

Jinsi ya Kuwasilisha Hadithi

Tunahimiza uwasilishaji kabla ya tarehe ya mwisho,kwa maana tutanakili hadithi kwa mtandao kadri tunavyozipata. Hili linajumuisha mitambo yetu ya kidigitali na kijamii, na pia mawasiliano ya mitandao ya kienyeji!

Ili hadithi yako kuchukuliwa kwa mkutano wa UNSG, ni lazima uitume kabla ya Julai 21.

Ufumbuzi wa asili ni nini haswa?

Kulingana na IUCN, “Ufumbuzi wa asili ni matendo ya kulinda, kusimamia kwa kudumu, na kurejesha asili, au mazingira yaliyobadilishwa ili kushughulikia changamoto za kijamii vyema na kikamilifu, wakati huo huo ukipeana faida kwa utu wema wa binadamu na viumbe hai. Ufumbuzi wa asili, kama vile urejesho wa misitu, mbuga na mabwawa ama juhudi za usimamizi endelevu wa ardhi, zinaweza kusaidia serikali na mikakati ya kufaa, inayolenga mbali, na yenye matumizi bora ili kukabiliana na kurekebisha mabadiliko ya tabia ya nchi.”

Kulingana na utafiti bora ulioongozwa na The Nature Conservancy, Ufumbuzi wa asili ya tabia ya nchi una uwezo wa kukabiliana na CO2 kwa asilimia 37% inayohitajika kufikia 2030 ili kwamba ifanikishe uwezekano wazaidi ya thuluthi mbili wa mizanijoto kubaki chini ya 2Co. Nyingi kati ya fumbuzi za asili zinawezesha faida zaidi ambazo zitaeneza urekebishaji wa tabia ya nchi, pamoja na kulinda dhidi ya mafuriko, kuongeza afya ya udongo na viumbe hai katika mazingira, pia kueneza kinga dhidi ya tabia ya nchi. Hata hivyo, jukumu la asili katika malengo ya tabia ya nchi halijatambulika vyema katika mazungumzo au katika fedha.       

Mifano ya fumbuzi za asili katika mabadiliko ya tabia ya nchi

 • Kuhifadhi na kurejesha misitu, mbuga na mabwawa, kurejesha misitu iliyoharibiwa au ardhi iliyofyekwa;

 • Kuhifadhi na kurejesha mazingira ya pwani, kama vile mabwawa ya chumvi, nyanja za nyasi bahari,matumbawe, na misitu ya mikoko;

 • Kuanzilisha mikakati ya kilimo endelevu kinachotunza kaboni ya udongo,na kuongeza uwezo wa kunyonya kaboni ya udongo.

 • Kuboresha usimamizi wa misitu ili kushirikisha viumbe hai na sayansi ya mazingira, na kuongeza uhifadhi na unyonyaji wa kaboni;

 • Kuhifadhina kuongeza sehemu asili mijini, ikiwemo kulinda na kujenga vipitio vinavyoiga asili ili kulinda viumbe hai.

Fumbuzi za asili za mabadiliko ya tabia ya nchi haitii ndani:

 • Kupanda miti ya aina moja katika shamba( yaani kutoa misitu halisi ili kuweka shamba la mawese);

 • Kugeuza mbuga asili kwa  njia bandia ili ziwe mandhari yenye misitu( upandaji miti);

 • Paa za kijani, au kuta za kijani, juu ya majengo;

 • Mitambo ya paneli za jua, ama aina nyingine ya miradi ya kawi safi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu fumbuzi za asili, angalia rasilimali hizi: Nature4Climate, The Nature-Based Solutions Initiative, IUCN.

Sheria na Masharti

Idhini na kutolewa kwa vyombo vya habari:

Unapowasilisha hadithi, unakubali kuwasilisha chini ya Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International licence (CC BY-NC 4.0). Inamaanisha kuwa Youth4Nature, na wengine, wana uhuru wa kusambaza na kunyakua wasilisho lako, kwa sababu zisizo za kibiashara, ili mradi mgao sahihi umewasilishwa. Angalia cheti cha leseni  kwa habari zaidi

Youth4Nature  watakuwa wanazambaza hadithi pindi ziingiapo katika jukwaa la mtandaoni la hadithi, katika mitambo ya kijamii, na pia katika mitambo ya kienyeji. Tutazisambaza pia katika mikutano husika ndani ya kongamano la UNSG mjini New York. lengo letu ni kuinua na kuimarisha sauti za vijana, kuongeza ueneaji wa hadithi hizi ili zipate kusambaa mbali, na kujenga sauti ya vijana kimataifa wanaotetea ufumbuzi wa asili.

Wote wanaoshiriki katika kampeni ya kuhadithia ya Youth4Nature lazima wapeane idhini kwamkataba wa  Media Release

Wanaoshiriki wana chaguo la kuwasilisha hadithi nusu bila kujulikana. Utaweza pia kushirikisha maelezo ya kibinafsi nasi, ila hadithi zako zitakuwa bila kujulikana pindi zitakapowekwa hadharani. Hadithi pia zitawasilishwa chini ya leseni ya the CC BY-NC 4.0 license.

Sera ya Faragha:

Youth4Nature ni mpango wa Climate Guides Foundation. Data tunayoipata kupitia Youth4Nature, ikiwemo kutokana na kampeni ya hadithi, imefungwa na Climate Guide`s Sera ya Faragha. Kwa kuwasilisha ombi, unaitikia kuwa umesoma na kukubaliana na sera hii. Climate Guides haitauza data yako ya binafsi. Ona sera kwa habari zaidi.

Mkutano wa UNSG:

Katibu Mkuu wa UN (UNSG) António Guterres ameandaa mkutano huu tarehe 23 Septemba 2019, ambapo anawataka viongozi kuja na mipango halisi na ya kweli ili kuimarisha michango ya kitaifa kufikia mwaka 2020, pamoja na kupunguza chafu ya gesi chafu kwa asilimia 45% katika muongo ujao, na pia uzalishaji wa sufuri wa chafu kufikia mwaka 2050. Mkutano huu utaleta pamoja serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, mamlaka za mitaa na shirika nyingine za mataifa.

Tunakadiria kuchagua wasemaji wa hadithi kadhaa ili wahudhurie mkutano kama moja ya wawakilishi wa Youth4Nature na kushirikisha hadithi zao. Tunatafuta hadithi zenye nguvy, zinazovutia kutoka kwa vijana wanaofanya jambo kuhusu ufumbuzi wa asili katika jamii zao. Ili kuchukuliwa, ni lazima:

 • Upatikane New York kutoka Septemba 18-27, 2019;

 • Uwe na uwezo wa kisheria wa kuingia Marekani;

 • Uonyeshe hamu ya kutaka kuchukuliwa kwa nafasi hii pindi unapowasilisha hadithi yako;

 • Uwasilishe hadithi yako kufikia Julai 21, 2019.

Tutakuwa tunawasiliana na wenye hadithi watakaochaguliwa kwa habari zaidi( ikiwemo nafasi ya muda wa mahojiano) kabla ya kuhakikisha chaguo. Tunatarajia kufidia gharama za kusafiri kwa wawakilishi watakao chaguliwa.

Muhimu: Iwapo utaamua kuwasilisha hadithi bila kujulikana, hautapata fursa ya kuhudhuria mkutano.


Maelezo ya mawasiliano

Iwapo una maswali yoyote kuhusu kampeni ya hadithi ya Youth4Nature, usikose kuwasiliana nasi kupitia y4n@climateguides.ca